|
Maendeleo ya Jamii
Jamii inayo fanikiwa ni
kama klabu ya Mpira yenye mafanikio. Kila mwanachama ana kazi ya
pekee, bado kila mmoja anwasaidia wengine kazi zao. Zaidi ya yote
kunakuwa na naodha anaye waongoza wachezaji wenzake na anaheshimika nao...
na kwa sababu ya mchezo wa umoja, jumla ni kubwa kuliko idadi ya watu
binafsi.
Kama huamini hilo, angalia mzinga wa nyuki, kilima cha mchwa au maringo
ya simba wakiwinda pamoja.
Miongoni mwa binadamu, kuna jamii nyingi, siyo wote wenye mafanikio,
wengine ni biashara, wengine wana vijiji, hospitali, shule au nchi.
Habari hizi ni za kuwasaidia kujenga umoja wenu kuwa jamii yenye
mafanikio. Kila kheri.
Shukrani za pekee kwa
msaada wa wa kurasa hizi ziwaendee Shirika la Uiingereza, Tearfund, kwa
nyongeza yao
ya "Miongozo ya Nguzo" inayoonekana hapa. Tearfund inatoa Jarida la
maendeleo la Nyayo. Linalo chapishwa kila baada ya miezi mitatu, kila
toleo linasisitiza juu ya maendeleo tofauti tofauti ya maendeleo ya
Jamii yakiwemo Maji, Afya, Elimu, Lishe na habari nyingine nyingi.
Kuangalia ( na kufungua) matoleo ya nyayo yaliyopita na kujua namna ya
kuyapata matoleo yajayo nenda
http://tilz.tearfund.org/publications/
kwenye mtandao huo huo utapata
mlolongo wa vitabu chini ya kichwa cha habari kikubwa vinavyoitwa "Mizizi"
kusaidia watumishi wa maendeleo.
 |