|
Mtandao huu hauwezi
kuwepo pasipo ukarimu, ujuzi na kazi bora ya mashirika kote ulimwenguni.
Ni sehemu ya kazi zao ambayo imejumuishwa hapa.
Kwa maelezo zaidi (na kudondoa) fuata maelekezo:
Kituo cha
Ushauri Nasaha, Lishe na Afya COUNSENUTH - (Centre for Counseling,
Nutrition and Health Care), ni shirika lisilo la serikali nchini Tanzania ambalo
dhamira yake ni kuendeleza afya, lishe na maisha ya Watanzania. Hasa kwa
kuendeleza huduma za kuzuia magonjwa, lishe bora, na ushauri nasaha katika
kiwango cha jamii. Lishe bora ni muhimu kwa kila mmoja katika kudumisha afya.
Na, kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, lishe bora laweza kuzuia maambukizo
zaidi na kuimarisha kinga yao. Kituo cha COUNSENUTH kimetambua kwamba ufahamu wa
lishe bora huchochewa na umaskini, tamaduni na mila, au hata itikadi na kukosa
maelezo sahihi. Kwa kushirikiana na mashirika mengine nchini Tanzania, kituo cha
COUNSENUTH kimeweza kuendeleza na kuratibu hitaji la lishe bora kwa Wananchi,
kupitia kwa ujumbe: Lishe bora ni muhimu katika kutunza na kuwasaidia watu walio
na virusi vya UKIMWI. Kituo hiki kina tarajia kupata wavuti hivi karibuni:
www.counsenuth.org
ECHO:
Mtandao kuhusu Suluhisho la tatizo la Njaa Duniani.
Kwa tuvuti la kimataifa tembelea:
www.echotech.org
Mtandao wa ECHO unatoa maelezo mengi ya dhamani. Shirika la ECHO halikadhalika huchapisha jarida kila baada ya
miezi mitatu `ECHO Development Notes'.
Forest & Landscape Denmark:
Shirika hili
limechapisha makala (katika Kingereza) na kutoa maelezo ya zaidi ya jamii 100 za
miti na majarida mengine muhimu. Kwa
maelezo zaidi tembelea: <Bwenyeza
hapa> - na panapo uwezekano bwenyeza `Kingereza'.
Kwa
mafunzo na maelezo au raslimali jaribu:
http://www.dfsc.dk/extensionstudy/index.html
HDRA
-
Henry Doubleday
Research Association http://www.hdra.org.uk/international_programme/index.htm
hufungua kurasa za huduma za kimataifa. Shirika la HDRA limejishughulisha na kilimo hai tangu
mwaka wa 1954 na kutoa maelezo kwa nchi za ng'ambo.
ICRAF- World Agroforestry
Centre (ICRAF) http://www.worldagroforestry.org/
utafungua tuvuti ya shirika maarufu ulimwenguni linaloongoza katika sayansi na
utafiti kuhusu `miti muhimu' na kilimo cha mseto kwenye mashamba madogo.
Shirika la ICRAF limeshirikisha
utafiti na mbinu bora za kisayansi katika kukabiliana na umaskini, njaa na
matatizo ya mazingira kote katika nchi za hari.
Maelezo muhimu na dharura yaweza kupatikana kwa kutazama
http://www.worldagroforestry.org/Sites/TreeDBS/aft.asp
KIOF-
Kenya Institute of
Organic Farming
[bwenyeza
hapa]
hujishughulisha na kilimo hai hasa katika nchi za hari.
 |